Raia mmoja wa Kimarekani mwenye asili ya Pakistan, amekamatwa kuhusika na jaribio lililoshindwa la kulipua bomu lililotegwa ndani ya gari katika uwanja mashuhuri wa Times Square mjini New York.
Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu usiku kutoka Washington, waziri wa sheria Eric Holder alimtaja mtuhumiwa kua ni Faisal Shahzad, mwenye umri wa miaka 30. Holder amesema Shahzad alikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa John F. Kennedy mjini New York masaa machache kabla ya kujaribu kupanda ndege kuelekea Dubai.
Vyombo vya habari vya Marekani vinaripoti kwamba huwenda Shahzad akafikishwa mahakamani Jumanne mchana.
Maafisa wa usalama wanasema Shahzad, aliyekua anaishi katika jimbo jiranbi la Connecticut, alitumia fedha taslimu kununua gari la aina ya Nissan Pathfindaer la 1993, lililotumiwa katika jaribio la bomu. Wanasema alinunua gari hilo kutoka mtu wa mji wa Bridgeport kupitia ukurasa wa tovuti. Inaripotiwa Shahzad alirudi Marekani karibuni kutoka Pakistan.
Mtu anayetuhumiwa akuhusika na jaribio lililoshindwa na bomu huko New York, Mmarekani mwenye asili ya Pakistan amekamatwa New York baada ya kupanda ndege kuelekea Dubai.