Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 04:17

Tillerson aishutumu China kwa "kukosa uwazi" barani Afrika


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson aliyeanza ziara ya siku nane barani Afrika.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson aliyeanza ziara ya siku nane barani Afrika.

Muda mfupi kabla ya kuanza  ziara yake ya kwanza ya kikazi barani Afrika, waziri wa mambo ya nje wa marekani Rex tillerson Tillerson aliishutumu China kwa "kuendeleza hali ya  kutegemea  katika sera zake kuelekea Afrika."

Tillerson alisema kwamba mtazamo wa marekani ni kuhamasisha utawala bora tofauti kabisa na muelekeo wa china unaohimiza hali ya kutegemea na kutumia mikataba isiyo yena uwazi kabisa, tabia zisizo fahamika za mikopo na mikataba ya rushwa inayotumbukiza mataifa katika madeni.

Katika hotuba yake ya kwanza akielezea sera za utawala wa Trump kwa Afrika, Tillerson alisema Marekani ina dhamira ya kupunguza vizuizi vya biashara na uwekezaji katika Afrika ambaye mshirika wake mkubwa sana wa biashara kwa sasa ni China.

Aidha Tillerson alisema kwamba Marekani ina nia ya dhati ya kujenga msingi madhubuti wa ushirikiano kati ya Marekani na Afrika.

Waziri Mkuu wa China, Li Keqiang na rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Waziri Mkuu wa China, Li Keqiang na rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

"Ili kuelewa ni wapi dunia inaelekea, tunapaswa kufahamu kuwa Afrika ndio mstakabal wa dunia," alisema Tillerson.

Mwanadiplomasia huyo alikuwa akizungumza katika chuo cha George Mason, kilicho nje kidogo ya mji wa Washington.

Kwa zaidi ya mwaka mmoja tangu rais Trump kuingia madarakani, bado hajamteua mwanadiplomasia mkuu kwa bara la Afrika, huku nchi za Afrika Kusini, Somalia, DRC na mataifa maengine matano ya bara hilo, yakisalia bila mabalozi.

Mwishoni mwa mwezi wa Januari mwaka huu, Trump aliibua utata na hisia mseto aliporipotiwa kutumia lugha chafu kwa nchi za Afrika pamoja na Haiti.

Lakini katika barua aliyowatumia viongozi wa Kiafrika, Trump alisema ana heshima kubwa kwa watu wa Afrika na kwamba waziri wa mambo wa nje Rex Tillerson atafanya ziara ndefu barani humo mwezi Machi.

Alhamisi, msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani Heather Nauert alisema ziara ya Tillerson kwa ujumla itaangazia masuala yafuatayo:

-Kutafuta ushirikiano katika kupambana na ugaidi

-uongozi bora

-Uimarishaji wa amani na usalama

-Kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji.

Ziara ya Tillerson ambayo itampeleka kwa mataifa matano; Kenya, Ethiopia, Djiboti, Chad na Nigeria, inafanyika wakati ambapo waziri wa Mambo ya nje wa Russia, Sirgei Lavrov antarajiwa kuzuru Ethiopia.

XS
SM
MD
LG