Mapema Ijumaa hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, baaada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake juu ya matumizi mabaya ya madaraka na kusababishia serikali hasara.
Katika utetezi wake, Tido alidai kuwa mchakato mzima wa kuingia ubia wa kuhamisha TBC kutoka katika mfumo wa analojia kwenda digitali ulifanywa na bodi ya TBC.
Kwa mujibu wa gazeti la Nipashe mahakama hiyo pia imesema kwamba mkataba anaodaiwa kusaini Tido kinyume cha sheria haukidhi vigezo vya kuitwa mikataba.
Tido alikuwa anakabiliwa na makosa matano, likiwemo la kuisababishia Serikali hasara ya Sh 887.1 milioni, katika kesi ya uhujumu uchumi namba 7/2018.
Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 7/2018, Tido alikabiliwa na mashtaka matano, mashtaka manne ni ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh887.1 milioni.</p>
Agosti 27, 2018 Mahakama hiyo ilimkuta Tido na kesi ya kujibu baada ya Hakimu Shaidi kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi watano wa upande wa mashtaka. Baada ya Tido kukutwa na kesi ya kujibu, alianza kujitetea.