Serikali ya Thailand ilitoa amri ya mwisho kuwataka wanawake, watoto, wazee na waandamanaji wasio na silaha kuondoa kutoka kambi yao kwenye wilaya ya biashara katika mji mkuu wa Bangkok ifikapo Jumatatu mchana.
Msemaji wa jeshi alisema Jumapili kuwa majeshi ya usalama yamepanga kuruhusu mashirika yasiyofungamana na upande wowote kama Msalaba Mwekundu kuingia kwenye eneo la waandamanaji ili kuwahimiza watu waondoke.
Hata hivyo risasi na milipuko ilitikisa eneo hilo Jumapili usiku wakati majeshi ya usalama yaliposhambulia wanamgambo waasi waliokuwa wanawarushia mawe, mabomu ya petrol na bunduki.
Matumaini ya kupatikana amani yalijitokeza pale viongozi wa waandamanaji kusema kwamba wako tayari kwa majadiliano Jumapili asubuhi. Chini ya pendekezo lao waandamanaji walivitaka vikosi vya usalama virudishwe nyuma na kuuruhusu Umoja wa Mataifa kua mpatanishi wa ugomvi wao.
Lakini msemaji wa serikali Panitan Wattanyagon alisema jeshi litaendelea na operesheni na upatanishi wa Umoja wa Mataifa hautakubalika. Wattanyagon alisema, serikali ya Thailand haina sera ya kuruhusu shirika lolote kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi. Akisema serikali ina uhuru wake na ufalme wa Thailand unaweza kutanzua matatizo yake