Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 02, 2025 Local time: 23:27

Ecuador yakumbwa na tetemeko kubwa la ardhi


Wafanyakazi wa kujitolea wakiutoa mwili kutoka nyumba moja iliyoharibiwa na tetemeko kubwa la ardhi huko Pedernales, Ecuador April 17, 2016.
Wafanyakazi wa kujitolea wakiutoa mwili kutoka nyumba moja iliyoharibiwa na tetemeko kubwa la ardhi huko Pedernales, Ecuador April 17, 2016.

Idadi ya vifo kutokana na tetemeko la ardhi nchini Ecuador inaendelea kuongezeka huku, Rais Rafael Correa akisema watu 272 tayari wamekufa, idadi hiyo ikitarajiwa kuongezeka. Zaidi ya watu 2,500 wamejeruhiwa.

Rais Correa alikuwa kwenye ziara nchini Italy Jumamosi wakati wa tukio hilo lakini akalazimika kukatiza ziara hiyo. Akizungumza kwenye mji ulioathiriwa zaidi wa Manta, Correa amesema kipaumbele cha sasa ni kutafuta walionusurika akiongeza kuwa kuna ushahidi kuwa baadhi yao wamekwama chini ya vifusi.

Amesema tetemeko hilo la 7.8 kwa kipimo cha rikta ndilo kubwa zaidi kuwahi kutokea nchini humo baada ya lile la mwaka wa 1949 mjini Ambato ambalo liliuwa maelfu ya watu. Wanajeshi wametumwa kwenye maeneo yalioathirika kwa shughuli za uokozi.

XS
SM
MD
LG