Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, Tedros wakati akizungumza kwa hisia nyingi kufuatia mapigano kuzuka tena kwenye eneo hilo Jumatano baada ya miezi kadhaa ya utulivu, amesema kwamba anasononeka kuona kwamba hana uwezo wa kuwasaidia watu wake ambao ni miongoni wa wakazi takriban milioni 6 waliokwama Tigray.
Amaongeza kusema kwamba kuna watu wengi wa jamii yake waliopo huko, na kwamba kamwe hawezi kuwasaidia licha yao kukumbwa na njaa. Hilo ni moja wapo ya maombi kuhusu Tigray, ambayo amekuwa akitoa kila anapozungumza na wanahabari kama kiongozi wa WHO.
Tedros amesema kwamba hatetei Tigray kwa kuwa yeye mwenyewe ni kutoka kabila la Tigrinya, mbali amekuwa akiangazia mizozo ya kibinadamu kwenye mataifa mengine pia kama vile Yemen, Syria, Ukraine na Congo. Hata hivyo katika siku za nyuma alisema kwamba huenda ulimwengu unasaidia watu wengine na kutelekeza watu wa Tigray kutokana na rangi ya ngozi yao.
Amesema kwamba hali ya Tigary ni ya kipekee kwa kuwa eneo hilo limenyimwa misaada muhimu inayohitaji ka kwa kwa watu wake, pamoja na kukatiwa mawasiliano na sehemu nyingine za ulimwengu. Mamlaka ya Tigray Jumatano imelaumu serikali ya Ethiopia kwa kuanzisha tena mashambulizi dhidi ya eneo hilo, baada ya hali ya utulivu kuwepo kwa karibu mwaka mmoja.