Mgombea wa urais Ted Cruz ametangazwa mshindi kwa chama cha Republican katika uchaguzi wa awali wa jimbo la Iowa, alipopata asilimia 28 mbele ya Donald Trump aliyepata asilimia 24.
Cruz ameibuka na ushindi katika jimbo hilo ambalo hutabiri mshindi wa atakaye peperusha bendera ya chama katika uchaguzi wa urais.