Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 22:57

Tanzania yaadhimisha miaka 60 ya uhuru wa nchi yake


Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania
Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania

Rais samia alisema nchi hiyo ina mfumo unaoruhusu raia kutumia uhuru wao wa kujieleza bila usumbufu wowote na kuongeza kuwa hali kwa waandishi wa habari imeboreka huku idadi ya mashirika ya habari yakiongezeka kutoka moja mwaka 1961 hadi mamia hivi leo

Tanzania iliadhimisha miaka 60 ya uhuru leo Alhamis huku Rais Samia Suluhu Hassan akisifu maendeleo ya nchi hiyo ingawa hofu inaongezeka kutokana na hali mbaya ya uhuru wa kisiasa katika taifa hilo la Afrika mashariki.

Katika hotuba yake kwa taifa mkesha wa maadhimisho hayo Rais Samia alisema mafanikio waliyoyapata katika miaka 60 iliyopita ya Uhuru yalichangiwa na utawala wa kidemokrasia na utawala wa sharia. Alisema kwamba nchi hiyo ina mfumo unaoruhusu raia kutumia uhuru wao wa kujieleza bila usumbufu wowote na kuongeza kuwa hali kwa waandishi wa habari imeboreka huku idadi ya mashirika ya habari yakiongezeka kutoka shirika moja mwaka 1961 hadi mamia hivi leo.

Koloni hilo la zamani la Uingereza lililojulikana kwa jina la Tanganyika lilijipatia uhuru mwaka 1961 na kuwa Tanzania baada ya kuungana na Zanzibar miaka mitatu baadae na kupitisha mfumo wa demokrasia ya vyama vingi mwaka 1992.

Lakini katika miaka ya hivi karibuni, vitisho vya uhuru wa msingi vimeongezeka nchini humo hasa chini ya utawala wa mtangulizi wa Samia, marehemu John Pombe Magufuli ambaye aliongoza kukandamiza vyombo vya habari, wanaharakati, na uhuru wa kujieleza.

Rais Samia Suluhu Hassan akila kiapo Machi 19, 2021.
Rais Samia Suluhu Hassan akila kiapo Machi 19, 2021.

Tangu Samia aingie madarakani Machi mwaka huu kufuatia kifo cha Magufuli amekuwa akitaka kuachana na baadhi ya sera za mtangulizi wake ambaye alipewa jina la “Jembe” kutokana na mtindo wake wa uongozi usiobadilika.

XS
SM
MD
LG