Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 05:13

Rais wa Tanzania atangaza mwelekeo mpya dhidi ya mapambano ya Covid-19


Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan baada ya kuaishwa Ikulu Dar es Salaam.March 19, 2021. (Tanzania State House Press/Handout via Reuters)
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan baada ya kuaishwa Ikulu Dar es Salaam.March 19, 2021. (Tanzania State House Press/Handout via Reuters)

Tanzania inatarajia kutoa mwelekeo mpya juu ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa COVID 19 ili kuendana na hali halisi ya mapambano hayo iliyopo duniani kwa sasa .

Msimamo huo umetolewa jijini Dar-es-salaam na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan wakati akiapisha watendaji mbalimbali wa serikali, na kusema kwamba Tanzania haipaswi kujitenga na dunia dhidi ya mapambano ya ugonjwa huu wa COVID 19 hivyo atarajia kuunda kamati itakayotoa mwelekeo wa nini kifanyike kuona namna ya kupambana na maradhi hayo

Katika hatua nyingine katika hotuba yake hiyo ya Jumanne Ikulu jijini Dar-es-salaam Rais Samia pia alitoa agizo kwa wizara ya Habari utamaduni sanaa na michezo kufungulia vyombo vyote vya habari vilivyofungiwa huku pia akiasa kufuatwa kwa sheria na kanuni zinazoongoza tasnia hiyo ya Habari.

Kufuatia kauli hiyo juu ya vyombo vya habari vilivyofungiwa jukwaa la wahariri Tanzania na Taasisi nyingine za habari hapa nchini wamepongeza hatua hiyo ya Rais lakini pia wakitaka kufuatwa kwa sheria na kanuni.

Rais Samia pia amerudia wito wake wa kuitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania kutoza kodi bila kudhulumu wafanyabiashara ambao amesema wengine wamekimbia kuwekeza nchini kutokana na kodi za dhuluma.

Watendaji walioapishwa Jumanne ni Makatibu wakuu na Manaibu katibu wakuu wa wizara mbalimbali ambao Rais amefanya uteuzi wao hivi karibuni. Rais Samia Hassan amechukua madaraka ya Urais hivi karibuni kufuatia kifo cha mtangulizi wake hayati John Pombe Magufuli Machi 17 mwaka huu.

XS
SM
MD
LG