Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:10

Tanzania Yaitaka UNHCR Kuwaondoa wakimbizi Wa Burundi


Wakimbizi wa Burundi wakiwa katika kambi ya Kigoma, Tanzania.
Wakimbizi wa Burundi wakiwa katika kambi ya Kigoma, Tanzania.

Serikali ya Tanzania siku ya Ijumaa ilihimiza shirika la kuhudumia wakimbizi katika Umoja wa Mataifa-UNHCR kuwarudisha haraka maelfu ya wakimbizi wa Burundi ambao inasema walitaka kurudi nyumbani kwao. Sauti ya Amerika-VOA ilizungumza na waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania, Mwigulu Nchemba na kutaka kujua muda kamili ambao serikali ya Tanzania iliipatia UNHCR katika zoezi la kuwarejesha wakimbizi hao.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:58 0:00

Waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania, Mwigulu Nchemba alisema kwamba zaidi ya wakimbizi 8,000 walishinikiza kurudi makwao.

Wakati huo huo mwezi Julai mwaka huu wa 2017 Rais wa Tanzania, John Magufuli alisitisha kwa muda usajili na uombaji uraia kwa maelfu ya wakimbizi wa Burundi wanaoishi nchini Tanzania. Zaidi ya warundi 240,000 wanaishi katika makazi ya muda huko Tanzania baada ya kukimbia ghasia za kisiasa zilizopelekea vifo kwenye nchi ya Burundi.

XS
SM
MD
LG