Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 12:50

Muhula wa Uongozi Afrika: Urais wa maisha utakuwa historia?


Rais kikwete wa Tanzania
Rais kikwete wa Tanzania

Wakati siku ya uchaguzi ikiwa inakaribia kwa kasi Oktoba 25 nchini Tanzania, Rais Jakaya Kikwete wa nchi hiyo anajitayarisha kuondoka madarakani baada ya kuongoza kwa mihula miwili.

Kulingana na katiba ya Tanzania Rais Kikwete hawezi kugombania tena urais kwani katiba hiyo inasema kila kiongozi ataongoza kwa mihula miwili tu ya miaka mitano. Tanzania imekuwa ikifuata urataratibu huo tangu mwaka 1985 wakati Rais Ali Hassan Mwinyi alipochukua uongozi baada ya kujiuzulu kwa Mwalimu Julius Nyerere ambaye aliongoza nchi hiyo kwa miaka 24.

Tangu wakati huo Rais Benjamin Mkapa aliongoza kwa awamu mbili kuanzia 1995 hadi 2005 na sasa Rais Jakaya Kikwete ambaye anaondoka madarakani baada ya kuongoza kuanzi 2005 hadi 2015.

Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi
Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi

Lakini Tanzania inaonekana kuwa tofauti na mataifa mengi Afrika ambako viongozi wanataka kubaki madarakani baada ya awamu zilizokubaliwa. Nchini Burundi kumezuka ghasia za kisiasa baada ya Rais Pierre Nkurunziza kuwania na kushinda urais kwa awamu ya tatu. Nchini Burkina Faso utawala wa miaka 27 wa Blaise Compaore ulimalizika kwa machafuko baada ya kiongozi huyo kutaka awamu nyingine.

Katika Jamhuri ya Congo, Raisd Denis Sassou Nguesso amependekeza mabadiliko ya katiba kubadili kiwango cha umri wa viongozi ambao ni miaka 70. Yeye ana umri wa miaka 72. Nchini DRC haijafahamika Rais Joseph Kabila ana mipango gani kuhusu uchaguzi wa mwakani ambapo atakuwa anamaliza awamu mbili.

XS
SM
MD
LG