Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 06, 2024 Local time: 08:52

Taliban inakaribisha mwaliko wa UN katika mkutano wa Qatar wa Juni 30


Amir Khan Muttaqi, waziri wa mambo ya nje wa Taliban. Sept. 19, 2022.
Amir Khan Muttaqi, waziri wa mambo ya nje wa Taliban. Sept. 19, 2022.

Makundi ya haki za binadamu yanakosoa kwa kuwatenga wawakilishi wanawake wa Afghanistan kwenye mkutano huo.

Taliban nchini Afghanistan wanaukaribisha mwaliko wa Umoja wa Mataifa katika mkutano wa kimataifa nchini Qatar baadae mwezi huu, wakiuchukulia kama utambuzi wa umuhimu wa utawala wao unaokuwa duniani.

Mkutano wa siku mbili wa Umoja wa Mataifa kati ya Taliban na wajumbe wa kimataifa kuhusu Afghanistan umepangwa kufanyika Juni 30 mjini Doha, mji mkuu wa taifa hilo la Ghuba, huku kukiwa na ukosoaji mkali kutoka kwa makundi ya haki za binadamu kwa kuwatenga wawakilishi wanawake wa Afghanistan.

Itakuwa ni kikao cha tatu cha kile kinachojulikana kama mchakato wa Doha, na watawala wa Afghanistan wenye msimamo mkali wamekubali kuhudhuria kwa mara ya kwanza.

Mkutano wa Doha utafanyika katika siku zijazo, na Imarati ya Kiislamu ya Afghanistan imealikwa rasmi kuhudhuria, Waziri wa Mambo ya Nje wa Taliban Amir Khan Muttaqi alitangaza katika taarifa kwa njia ya video iliyotolewa na ofisi yake Jumatatu.

Forum

XS
SM
MD
LG