Tetemeko la kwanza la Jumatatu jioni lenye ukubwa wa 5.5 lilishuhudiwa kwenye kaunti ya mashariki ya Hualien, ambako ni kitovu cha lile la Aprili 3, likifuatiwa na matetemeko madogo.
Tetemeko kubwa zaidi lilishuhudiwa saa kadhaa baadaye likiwa na ukubwa wa 6.3 kulingana na kituo cha hali ya hewa cha Taipei, dakika chache baada ya jingine kutokea lenye ukubwa wa 6.0 kwa vipimo vya rikta. Maafisa wa kaunti ya Hualien wamesema kuwa majengo mawili yaliyoharibiwa wakati wa tetemeko la Aprili 3, sasa yameporomoka, kufuatia tetemeko la mapema Jumanne.
Kituo cha hali ya hewa kimesema kuwa matetemeko ya sasa ni mwendelezo wa hilo la Aprili 3. Hakuna vifo vilivyoripotiwa kwenye matukio hayo ya karibuni, ingawa shule na ofisi huko Hualien zimefungwa leo Jumanne. Tetemeko la Aprili 3 linasemekana lilikuwa na nguvu zaidi baada ya lile la vipimo vya 7.7 lililotokea miaka 25 iliyopita na kuuwa watu 2,400, pamoja na kuharibu maelfu ya majengo.
Forum