. Hatua hiyo ni kutokana na kuongezeka maradufu kwa maambukizi ya corona yanyotokana na aina mpya ya virusi omicron.
Tangazo hilo ni pigo kubwa kwa wafanyabiashara wa meli hizo waliorejea kazini mwezi Juni baada ya kusitisha shughuli zao kwa muda mrefu tangu kuzuka kwa janga la corona.
CDC imekuwa ikifanya uchunguzi wa maambukizi kwenye meli hizo wakati takriban asilimia 10 ya abiria wakipatikana kuwa na virusi vya corona.
Hisa za makampuni ya cruise ya Carnival Corp, Norwegian Cruise Line Holdings Ltd na Royal Caribbean Group zinasemekana kushuka kwa asilimia 1 baada ya tangazo la CDC. Kampuni ya Norwegian Cruise hata hivyo imesema kwamba inaamini abiria wake kwenye meli wapo salama zaidi ya kutopata maambukizi ya covid wakilinganishwa na watu walioko kwenye nchi kavu.
CDC imesema kwamba watu walioko kwenye meli tayari wanahitajika kufanya vipimo siki 3 hadi 5 baada ya kukamilisha safari huku wakijiweka kwenye karantini kwa siku 14.