Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 10:50

Utafiti wabaini Wapalestina hawaziamini sera za Trump


Rais Mahmoud Abbas
Rais Mahmoud Abbas

Tafiti inaonyesha kuwa wengi wa Wapalestina wanaamini kuwa sera za Rais Donald Trump zitapelekea misuguano kati ya Waisraeli na Wapalestina au kukwama kwa mazungumzo huko Mashariki ya Kati.

Katika utafiti unaojulikana kama "Opinion Poll" uliyofanywa Jumanne na Kituo cha Palestina kinachosimamia sera na tafiti kimesema kuwa ni asilimia 9 tu ndio wanaamini kuwa Trump ataweza kuanzisha upya mazungumzo kati ya Israeli na Palestina.

Tafiti hiyo iliyo wahusisha wasailiwa 1,270 ilikuwa inaonyesha kuwa inawezekana kuwa watu wengi zaidi kwa asilimia tatu wanakubaliana na sera za Trump au pengine inaweza kuwa hawakubaliani naye kwa asilimia tatu zaidi juu ya kuanzisha upya mazungumzo.

Matokeo ya tafiti hii yalikuwa yamechapishwa wakati Rais wa Palestina Mahmoud Abbas alipo mpokea mjumbe wa Trump, Jason Greenblatt ili kujadili juhudi za kutafuta suluhisho la amani. Greenblatt alikutana Jumatatu na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu.

Taarifa ya Marekani imesema kuwa Greenblatt amemwambia Netanyahu kuwa Trump anamatumaini ataweza kutafuta utaratibu wa suala la ujenzi wa makazi utaokuwa unalingana na lengo la Marekani la kufikia makubaliano ya Amani. Mjumbe huyo amesema Trump anapenda kunyanyua na kukuza uchumi wa Palestina.

XS
SM
MD
LG