Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 08:35

Syria yasema Israel imefanya shambulizi Damascus


Shambulizi la angani lililofanywa na Israeli huko Kafr Sousa katika mji mkuu wa Syrian Damascus February 21, 2024.
Shambulizi la angani lililofanywa na Israeli huko Kafr Sousa katika mji mkuu wa Syrian Damascus February 21, 2024.

Hakuna uthibitisho kuwa mashambulizi hayo yanatokea Israeli.

Televisheni ya serikali ya Syria iliripoti kwamba makombora kadhaa yalipiga kitongoji cha magharibi cha Kfar Sousseh lakini haikufafanua au kusema ni watu wangapi waliouawa.

Kituo cha redio kinachoiunga mkono serikali cha Sham FM kilisema shambulizi hilo lilipiga jengo karibu na shule ya Iran.

Rais wa Syria, Bashar al-Assad
Rais wa Syria, Bashar al-Assad

Rami Abdurrahman, ambaye anaongoza Shirika la Kufuatilia Haki za Binadamu la Syria, mfuatiliaji wa vita vya upinzani yenye makao yake nchini Uingereza, alisema watu wawili waliouawa walikuwa ndani ya ghorofa lakini hakutoa vidokezo vyovyote kuhusu utambulisho wao.

Israel mara chache haikubali hatua zake nchini Syria, lakini imesema inalenga kambi za wapiganaji wanaoungwa mkono na Iran, kama vile Hezbollah ya Lebanon, ambayo imetuma maelfu ya wapiganaji kuunga mkono vikosi vya Rais wa Syria Bashar Assad.

Forum

XS
SM
MD
LG