Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 02, 2025 Local time: 19:10

Syria imedai kushambuliwa na Israel


Eneo la makazi nchini Syria
Eneo la makazi nchini Syria

Syria imesema kwamba mashambulizi ya anga ya Israel yamepiga majengo ya makazi ya watu mjini Damascus.

Shirika la habari la serikali ya Syria limeripoti kwamba watu wawili wamefariki kwenye mashambulizi hayo katika mji wa Kfar Sousseh, ambao pia ni makao makuu ya ulinzi na jeshi.

Jeshi la Israel, ambalo limetekeleza mashambulizi kadhaa ndani ya Syria katika miaka ya hivi karibuni, halijatoa taarifa yoyote kuhusu shambulizi hilo

Ni nadra sana kwa Israel kukiri kutekeleza mashambulizi ndani ya Syria, lakini imesema kwamba hatua zake ni kuyalenga vikosi vinavyoungwa mkono na Iran.

Shambulizi la anga la Februari mwaka 2023, katika ujirani huo huo kama hili la leo Jumatano, liliua wataalam kadhaa wa kijeshi wa Iran.

Forum

XS
SM
MD
LG