Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 07:32

Sultan wa zamani wa Zanzibar Jamshid bin Abdullah arudi Oman


Jamshid bin Abdullah, Sultan wa zamani wa Zanzibar akiwasili London baada ya kupinduliwa na John Okello 1964.
Jamshid bin Abdullah, Sultan wa zamani wa Zanzibar akiwasili London baada ya kupinduliwa na John Okello 1964.

Aliyekuwa Sultan wa Zanzibar, Jamshid bin Abdullah ambaye tangu aondolewe mamlaka mwaka 1964 amekuwa akiishi nchini Uingereza amekwenda Muscat baada ya serikali ya Oman kukubali ombi lake la kutaka kustaafu nchini Oman.

Jamshid mwenye umri wa miaka 91 aliondolewa madarakani mwaka 1964 katika mapinduzi yaliyoongozwa na wanaharakati wa kiafrika na tangu wakati huo amekuwa akiishi nchini Uingerezaz katika mji wa Portsmouth kwa zaidi ya miaka 50 sasa. Alirithi usultani kutoka kwa baba yake Abdullah bin Khalifa mwezi Julai mwaka 1963.

Serikali ya Oman haikutangaza hadharani kuhusu kustaafu kwa mtawala huyo wa zamani wa Zanzibar. “Ni suala binafsi na hatutaki kutangaza hivyo,” afisa mmoja wa serikali ya Oman amesema kwa misingi ya kutotajwa jina.

Awali Jamshid mara kadhaa alinyimwa ruhusa ya kustaafu nchini Oman kwasababu za kiusalama. Maelfu ya waliokuwa katika utawala wake wa zamani wanaishi nchini humo baada ya kupewa uraia katika miaka ya 1970 na 1980.

Jamshid anaelezewa ana uhusiano wa kidugu za mtawala wa sasa wa Oman, Haitham bin Tarek, ambaye wote wanatokea katika ukoo wa kifalme.

Watu kutoka Zanzibar wanaiona Oman lama sehemu ya makazi yao ya asili kwa vile kisiwa hicho kilitawaliwa na Oman kati yam waka 1698 mpaka 1890. Na mwaka 1890 Uingereza iliilazimisha Zanzibar kuwa chini ya Himay ya Kiingereza na kisiwa hicho kilijitenga na Oman na kuwa kisiwa huru kilichoongozwa na Sultan wa hapo hapo Zanzibar.

Jamshid ataungana na dada yake, kaka na watoto wake saba ambao wamekuwa wakiishi nchini Oman tangu miaka ya 1980. Haruhusiwi kurejea Zanzibar.

“Tuna furaha kubwa kwaba Sultan Jamshid atakuwa na sisi katika nchi hii katika siku zake za mwisho. Sisi pia tunaishukuru serikali ya Oman kwa kumpa ruhusa ya kustaafu hapa, kwa kweli nadhani ni kwasababu za kibinadamu,” amesmea Yusuf Al-Shibl, mwenye umri wa miaka 74, raia wa Oman ambaye alizaliwa Zanzibar na hivi sasa anaishi Muscat.

XS
SM
MD
LG