Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 08:59

Sudan yazuia misaada ya kibinadamu


wakazi wakiwa wamekusanyika nje ya makao makuu ya pfisi za umoja wa mataifa huko Kadugli
wakazi wakiwa wamekusanyika nje ya makao makuu ya pfisi za umoja wa mataifa huko Kadugli

Shirika la UN la misaada limesema wafanyakazi wameweza kuingia kwenye maeneo pekee ambayo makundi ya kutoa misaada yana ofisi zake


Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya kibinadamu limesema serikali ya Sudan inatoa nafasi ndogo ya kufika katika mji ulio mpakani wenye mgogoro kusini mwa nchi hiyo na kwamba wafanyikazi wa kutoa misaada hawaruhusiwi kuingia katika maeneo mengi katika mji huo.

Ofisi ya umoja wa mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu imesema wafanyakazi wake wa msaada wameweza kuingia Kadugli mji mkuu wa jimbo lenye mvutano la Kordofan.

Hata hivyo shirika hilo limesema wafanyakazi wameweza kuingia kwenye maeneo pekee ambayo makundi ya kutoa misaada yana ofisi zake lakini hawana uwezo wa kugawa msaada kwa watu wa mji huo.

Umoja wa Mataifa pia umesema ofisi zake zote huko Kadugli zimevamiwa .

XS
SM
MD
LG