“Viongozi wote wa vuguvugu la the Forces for Freedom and Change, ambao walikuwa kizuizini katika wiki za karibuni, wameachiliwa,” wakili Azhari al-Haj ameiambia AFP.
The Forces for Freedom and Change (FFC), ni kundi kubwa la kiraia la Sudan lililoondolewa madarakani kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya tarehe 25 Oktoba yaliyoongozwa na mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan.
Mapinduzi hayo yalikwamisha mchakato wa kurejesha utawala wa kiraia ulioanzishwa baada ya kiongozi wa muda mrefu Omar al Bashir kuondolewa madarakani mwaka wa 2019.
Wajumbe wa FFC walioachiliwa huru ni pamoja na Babiker Faisal, Wagdi Saleh na Taha Othman, wakili wao amesema, vile vile mjumbe wa zamani wa Baraza kuu la uongozi, Mohamed al-Fekki.
Aliyekuwa waziri wa masuala ya baraza la mawaziri kabla ya mapinduzi Khaled Youssef, aliachiliwa Jumanne.