Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:23

Sudan yatangaza dharura ya kitaifa kutokana na mafuriko


Mafuriko nchini Sudan.
Mafuriko nchini Sudan.

Baraza la usalama na ulinzi la Sudan limetangaza dharura ya kitaifa ya miezi mitatu kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na ambazo zimesababisha vifo vya takribana watu 100 kufikia sasa. Shirika la Habari la serikali SUNA liliripoti mapema Jumamosi.

Waziri wa wafanyakazi na maendeleo ya kijamii wa Sudan, Lena El Sheikh, amesema kwamba pamoja na vifo hivyo, watu kadhaa pia wamejeruhiwa kutokana na mafuriko hayo, huku Zaidi ya watu laki tano wakiathiriwa kwa njia moja au nyingine.

Shirika hilo la SUNA aidha limeripoti kwamba takriban nyumba laki moja zimeharibiwa kabisa na mafuriko hayo.

Kwa mujibu wa waziri Sheikh, viwango vya mvua na mafuriko mwaka huu vimezidi vile vya kati ya mwaka wa 1946 na 1988, na kuna kila dalili kwamba vitaendelea kupanda hata Zaidi.

Baraza hilo pia limeunda kamati maalum ya kushughulikia janga hilo, ambayo itaongozwa na Waziri Sheikh.

XS
SM
MD
LG