Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 07:23

Sudan Kisini yakabiliwa na uhaba wa chakula miaka 10 baada ya uhuru


Mama akisuburi msaada wa chakula Sudan kusini kwenye picha ya awali
Mama akisuburi msaada wa chakula Sudan kusini kwenye picha ya awali

 Ingawa imekuwa miaka 10 tangu Sudan kusini kujipatia uhuru wake,wakazi wangali wanakabiliwa na tatizo la usalama wa chakula licha ya kuwepo ardhi kubwa inayofaa kwa kilimo.

Ripoti kutoka shirika la chakula ulimwenguni, WFP, iliyotolewa mwezi uliopita inasema kuwa asilimia 60 ya wakazi milioni 7.2 wa Sudan Kusini wakabiliwa na ukosefu wa usalama wa chakula kwenye robo ya kwanza ya mwaka huu.

Kulingana na mwenyekiti wa taasisi ya kiuchumi ya Sudan Kusini, Laku Likang, taifa hilo linaagiza asilimia 80 ya chakula kutoka mataifa ya nje. Vyakula kama mboga na nyanya miongoni mwa vingine kwa mfano huagizwa kutoka Uganda.

Wakati akizungumza kipindi cha VOA cha South Sudan in Focus, Lukang amesema kwamba tangu taifa hilo lijipatie uhuru wake, bado halijaweza kubuni viwanda vya kutengeneza bidhaa kama vile mafuta ya kupikia au hata sukari.

Ameongeza kusema kuwa licha ya taifa hilo kuwa na mafuta ghafi, fedha zinazopatikana zinahitajika kununua vifaa muhimu vya kilimo kama matrekta ili kuongeza uzalishaji wa chakula.

XS
SM
MD
LG