Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 04:00

Mzozo mwingine waibuka kati ya Sudan kaskazini na kusini


Nyumba zikichomwa moto huko Abyei baada ya majeshi ya Sudan kaskazini kukalia kimabavu mkoa wenye utajiri wa mafuta wa Abyei.
Nyumba zikichomwa moto huko Abyei baada ya majeshi ya Sudan kaskazini kukalia kimabavu mkoa wenye utajiri wa mafuta wa Abyei.

Serikali ya Sudan kaskazini inaitaka kusini iondoe majeshi yake kutoka kwenye majimbo ya Blue Nile na Kordofan ifikapo Jumatano.

Serikali ya Sudan kaskazini inaitaka kusini iondoe majeshi yake kutoka kwenye majimbo mawili muhimu ya mpakani ifikapo Jumatano.

Dai hilo limeripotiwa na vyombo vya habari vya Sudan, linahusu majimbo ya Blue Nile na Kordofan kusini. Majimbo hayo yako katika mpaka kati ya Sudan kaskazini na kusini, kama ilivyo kwa mkoa wenye mzozo na wenye utajiri wa mafuta wa Abyei, ambapo majeshi ya kaskazini yanaukalia kimabavu kwa zaidi ya wiki moja iliyopita.

Majimbo hayo mawili hivi sasa yapo chini ya udhibiti wa kaskazini lakini yalikuwa maeneo ya mapambano wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa muda mrefu kati ya Sudan kaskazini na kusini.

Kusini inakaribia kujitangaza uhuru Julai 9 baada ya kupiga kura ya kujitenga kutoka kaskazini katika kura ya maoni iliyofanyika mwezi Januari.

Wachambuzi wanaonya kusini huwenda ikachagua kupigania majimbo ya Blue Nile na Kordofan kusini, baada ya kusema haitaruhusu mgogoro wa Abyei kuwarudisha katika vita.

Jumapili kundi la kimatiafa la uangalizi lilionya kwamba majeshi ya Sudan kaskazini yanaonekana kuuharibu mji mkuu wa Abyei, katika kile kinachoonekana ni kitendo cha uhalifu wa vita.

Mradi wa Satellite Sentinel pia ulisema ulikuwa na picha zinazoonyesha msururu wa vifaru, magari makubwa, makombora na magari ya vita huko Abyei. Inasema majeshi yana uwezo wote wa kusonga mbele haraka.







XS
SM
MD
LG