Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 10:59

Stormy Daniels anaendelea kutoa ushahidi wake dhidi ya Trump


Stormy daniels, muigizaji wa filamu za ngono.
Stormy daniels, muigizaji wa filamu za ngono.

Daniels aliliambia jopo la majaji 12 kuwa anamchukia Trump na anataka rais huyo wa zamani Marekani awajibishwe

Muigizaji wa filamu za ngono Stormy Daniels anakabiliwa na maswali zaidi leo Alhamisi katika kesi ya Donald Trump mjini New York kuhusu madai yake ya kukutana naye kimapenzi mwaka 2006 na madai kwamba alimlipa dola 130,000 mwaka 2016 ili kukaa kimya kuhusu hilo wakati wapiga kura wakielekea kwenye uchaguzi katika mafanikio yake ya kuwania kuingia White House.

Daniels aliliambia jopo la majaji 12 siku ya Jumanne kwamba anamchukia Trump, anataka rais huyo wa zamani awajibishwe na kupelekwa jela kama atapatikana na hatia. Trump, anakuwa rais wa kwanza wa zamani kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu, amekanusha maelezo ya Daniels ya jaribio la usiku mmoja katika ziara yake ya gofu ya watu mashuhuri katika Ziwa Tahoe kwenye jimbo la Nevada na mashtaka yote 34 anayokabiliwa nayo.

Kama atapatikana na hatia, anaweza kuwekwa kwenye kipindi cha uangalizi au kufungwa hadi miaka minne. Anashutumiwa kwa kudanganya rekodi za biashara katika kampuni yake ya Trump kwa mali isiyohamishika ili kuficha malipo ya dola 130,000 kwa Daniels kwa kutuma hundi za kila mwezi mwaka 2017 kwa Michael Cohen, wakili wa zamani wa Trump na mrekebishaji wa masuala yake ya kisiasa ambaye alituma pesa hizo kwa Daniels kutoka kwa mkopo wake wa kibinafsi wa nyumba.

Forum

XS
SM
MD
LG