Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Julai 05, 2024 Local time: 02:18

Sri Lanka kuokoa dola bilioni 5 kufuatia marekebisho ya madeni nchini humo


Rais Ranil Wickremesinghe wa Sri Lanka
Rais Ranil Wickremesinghe wa Sri Lanka

Taifa hilo katika kisiwa lilishindwa kukopa kwa nchi za kigeni mwaka 2022 wakati wa mgogoro wa kiuchumi usio wa kawaida

Sri Lanka itaokoa dola bilioni 5 kufuatia marekebisho ya madeni yake ya nchi mbili, ambayo mengi yanadaiwa na China kwa kupunguzwa kwa viwango vya riba na ratiba ndefu za ulipaji, Rais wa nchi hiyo alisema Jumanne.

Taifa hilo katika kisiwa lilishindwa kukopa kwa nchi za kigeni mwaka 2022 wakati wa mgogoro wa kiuchumi usio wa kawaida ambao ulisababisha miezi kadhaa ya uhaba wa chakula, mafuta na dawa. Rais Ranil Wickremesinghe alisema makubaliano yaliyofikiwa wiki iliyopita yamewezesha kusitishwa kwa malipo ya madeni hadi mwaka 2028 na kuongeza muda wa mikopo kwa miaka minane na kupunguza viwango vya riba kwa wastani wa asilimia 2.1.

Wickremesinghe alisema wakopeshaji wa nchi mbili wakiongozwa na China, mkopeshaji mkubwa zaidi wa serikali hawakukubali kuchukua mkopo wao, lakini masharti yaliyokubaliwa yataisaidia Sri Lanka.

Forum

XS
SM
MD
LG