Trump amesema “sisi tuko karibu, karibu mno” kupitisha mswada uliotayarishawa na chama tawala uliokuwa umekusudiwa kuchukua nafasi ya sheria ya afya (ACT) ambayo ilisainiwa na Rais mstaafu Barack Obama miaka saba iliyopita.
Spika wa Bunge Paul Ryan amekuwa akiongoza juhudi za kupitisha pendekezo la serikali la kuiondoa Obamacare, na hatua ya uongozi kuondosha mswada huo Ijumaa ilikuwa ni dalili ya kuemewa kwa spika na Trump baada ya kukosa kura stahiki.
Spika ambaye ni afisa wa juu wa Chama cha Republikan katika Bunge, alikuwa ameahidi mwezi huu kwamba timu yake itakusanya kura 218 ambazo ni muhimu kupitisha sheria hiyo mpya: “Sisi sote tutakuwa na kura 218 wakati suala hili likija bungeni, ninaweza kuwahakikishia hilo.”
Baada ya mswada huo kuondolewa na Rais, Ryan alitangaza, “Tutaendelea kuishi na sheria ya Afya, Obamacare kwa kipindi kirefu kijacho.