Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 14:00

Waziri Mkuu wa Somalia achagua baraza la mawaziri


Waziri Mkuu Hassan Ali Khaire
Waziri Mkuu Hassan Ali Khaire

Baraza jipya la Mawaziri Somalia limepata Waziri wa udhibiti wa maafa ambae atashughulikia ukame ambao umeikumba nchi hiyo na kuwaacha watu zaidi ya milioni sita wakihitajia msaada.

Waziri Mkuu Hassan Ali Khaire amezindua baraza lake hilo Jumanne Mogadishu. Kwa mara ya kwanza katika historia ya Somalia, wanawake kadhaa ni miongoni mwa wale waliochaguliwa, akiwemo waziri wa udhibiti wa maafa, Maryan Qasim Ahmed.

Khaire ameteua mawaziri 68 kwa jumla, wengi wao walikuwa katika serikali iliyotangulia

Wasomali wengi walikuwa wanategemea baraza dogo, hasa wakizingatia ahadi ya Rais Mohammed Abdullahi Mohammed kuendesha serikali yenye mafanikio na kuzuia rushwa.

“Ukweli ni kuwa baraza la mawaziri kubwa haliwezi kukidhi matarajio makubwa ya wananchi kutoka kwa viongozi waliokuwa madarakani,” amesema mchambuzi wa Kisomali alioko Virginia Abdiqafar Abdi Wardhere.

“Tunaamini kuwa baraza hili jipya haliakisi mageuzi ambayo tulikuwa tunayategemea kutoka kwa rais na waziri mkuu,” amesema Dini Mohamed Dini, Mwenyekiti wa Taasisi ya Kiraia ya Jumuiya ya Somalia.

“Tulikuwa tunatarajia sura mpya, zenye kuaminika, na wataalamu, pia watu ambao wanauwezo wa kuongoza taifa katika mwelekeo sahihi, lakini sura za zamani katika baraza hilo zinaonyesha ni kinyume cha hivyo.”

Qasim Ahmed alikuwa katika serikali iliyotangulia ni waziri wa maendeleo ya watu na huduma za umma.

Mteule wa Khaire anae shikilia wizara ya fedha, ni mchumi Abdirahman Duale Beyle, ambae alikuwa ni waziri wa mambo ya nje katika utawala uliopita.

Waziri wa mambo ya nje alieteuliwa na Khaire ni Yusuf Garad Omar, Raia pacha wa Uingereza na Somalia ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa idhaa ya Kisomali –BBC.

Wateule wote hawa ni lazima wapitishwe na bunge la Somalia.

Bunge lilimchagua Rais Mohammed, ambae ni maarufu kwa jina la Farmajo, kwa kipindi cha miaka mitano mwezi uliopita.

Farmajo ameahidi kuiimarisha nchi ya Pembe ya Afrika, ambayo haijawahi kuwa na serikali imara kwa zaidi ya miaka 25.

XS
SM
MD
LG