Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:19

UNICEF yaingia maeneo ya al-Shabab kutoa misaada


UNICEF imesafirisha tani tano za msaada wa chakula kwa ajili ya watoto wenye utapiamlo nchini Somalia kufuatia ukame uliolikumba eneo la pembe ya Afrika
UNICEF imesafirisha tani tano za msaada wa chakula kwa ajili ya watoto wenye utapiamlo nchini Somalia kufuatia ukame uliolikumba eneo la pembe ya Afrika

Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka miwili, Umoja wa Mataifa imepeleka misaada katika baadhi ya sehemu za Somalia zinazodhibitiwa na wanamgambo wa kundi la al-Shabab.

Msemaji wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa-UNICEF ameiambia Sauti ya Amerika, Idhaa ya Kisomali kwamba shirika hilo lilisafirisha tani tano za misaada kwenda kwenye mji wa Baidoa, Jumatano. Amesema misaada hiyo ni pamoja na madawa na lishe na maji. Misaada hiyo ni kwa ajili ya watoto wenye utapiamlo mbaya nchini Somalia kufuatia ukame uliolikumba eneo la pembe ya Afrika.

UNICEF ilisitisha kwa muda kupeleka misaada kwa njia ya anga kuelekea maeneo yaliyodhibitiwa na al-Shabab mwaka 2009 kwa sababu ya vitisho kutoka kwa wanamgambo. Shirika hilo liliendelea kupeleka baadhi ya misaada kwa njia ya barabara.

Wiki iliyopita kundi la al-Shabab lilisema linayakaribisha makundi ya kibinadamu kurudi katika maeneo wanayoyadhibiti.

Pia Jumatano, Umoja wa Afrika ulisema unafanya kazi na walinda amani wa Umoja wa Afrika kuongeza usalama nchini Somalia kuhakikisha kwamba msaada wa kibinadamu unafika kwa wasomali ambao wanahitaji msaada huo.

Msemaji wa Umoja wa Afrika, El-Ghassim Wane alisema Umoja wa Afrika unasaidia kulinda kote njia ya majini na kiwanja cha ndege na kurahisisha kuleta vifaa vya msaada.Pia alisema Rais wa zamani wa Ghana Jerry Rawlings karibuni ataitembelea Somalia kutathmini hali ya Umoja wa Afrika.


XS
SM
MD
LG