Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 02, 2025 Local time: 22:14

Polio yaangamizwa Somalia.


Mtoto apatiwa chanjo dhidi ya ugonjwa wa kupooza Somalia.
Mtoto apatiwa chanjo dhidi ya ugonjwa wa kupooza Somalia.

Baada ya miaka mingi ya kampeni za chanjo dhidi ya ugonjwa wa kupooza , WHO pamoja na wizara ya afya kwa pamoja wametangaza Somalia kuwa huru dhidi ya ugonjwa huo. Dkt Ghulam Popal ambae ni mratibu wa WHO nchini Somalia anasema kuwa kwa mwaka mmoja sasa, hakuna kesi mpya iliyoripotiwa na kwamba anatumaini mfumo wa ufuatiliaji na uangalizi uliopo utaendelea, na baada ya miaka mitatu watatangaza Somalia kuwa nchi isio na ugonjwa wa kupooza tena.

Kwa miaka mingi, maafisa wa afya wa Somalia kwa kushirikiana na mashirika ya umoja wa mataifa na WHO wamewapatia chanjo mamilioni ya watoto wa Somalia, wengi wao wakiwa chini ya miaka mitano. Virusi vya ugonjwa huo vimeathiri watoto wengi katika maeneo ya kusini ya kati mwa Somalia ambalo lilikuwa limeshikiliwa na kundi la kigaidi la al-Shabab.

Waziri wa afya wa Somalia, Hawa Hassan Mohamed, anasema kesi 189 za ugonjwa wa huo zilirekodiwa nchini humo mwaka wa 2013. Hio ndio ilikuwa idadi kubwa zaidi ya kesi zote ulimwenguni. Ameongeza kusema kuwa wana Imani na maendeleo yaliopatikana na kwamba wataendelea kuongeza juhudi za kupatiana chanjo na kuwahamasisha wazazi. Ugonjwa wa kupooza- polio hautibiki ila unazuilika.

XS
SM
MD
LG