Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 02, 2025 Local time: 20:13

Serikali ya Somalia yagomea mkutano wa Nairobi


Rais wa Somalia, Sheikh Sharif Sheikh Ahmed
Rais wa Somalia, Sheikh Sharif Sheikh Ahmed

Wanadiplomasia wa kimataifa, mawaziri wa serikali, makundi yenye silaha na wanasiasa wapo mjini Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya mkutano juu ya hali ya baadaye ya kisiasa nchini Somalia.

Mkutano huo pia unahudhuriwa na wawakilishi wa majimbo yaliyojitenga kama vile Puntland na Glamudug pamoja na Ahlu Sunna Wal Jamaa, kundi lenye silaha lililojiunga na serikali ya mpito ya Somalia. Lakini kilichoonekana kukosekana kutoka kwenye mkutano huo ni wawakilishi wa serikali yenyewe.

Muda mfupi baada ya mkutano kutangazwa mwezi Machi, Waziri wa Ulinzi wa Somalia, Abdihakim Fiqi, alisema mazungumzo hayo yataharibu maendeleo yaliyofanywa na serikali ya Somalia zaidi ya miezi kadhaa iliyopita na alieleza kwamba wawakilishi kutoka serikali ya mpito hawatashiriki.

Wote Rais Sheikh Sharif Sheikh Ahmed na Waziri Mkuu Mohammed Abdullahi Mohammed walirudia matamshi ya Fiqi. Waziri Mkuu, katika ziara yake ya hivi karibuni kwenda Nairobi kukutana na Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, aliwaambia waandishi wa habari kwamba mkutano wowote wa aina hiyo utatakiwa kuongozwa na Somalia mjini Mogadishu.

Kwa mujibu wa mchambuzi wa masuala ya kisiasa Rashid Abdi wa kundi linalohusika na migogoro ya kimataifa lenye makao yake Brussels, mtazamo wa TFG unaonyesha uhusiano uliodhoofika kati ya viongozi wa Somalia na jumuia ya kimataifa.

XS
SM
MD
LG