Afisa mkuu wa serikali ya Somalia, Alhamisi aliiambia VOA kwamba serikali ya Somalia “imelinda na kutenga” wanajeshi wote wanaohitajika kutoka nchi nyingine nne zinazochangia wanajeshi wa AU, Burundi, Djibouti, Kenya na Uganda, kushiriki katika Ujumbe wa Msaada na Utulivu wa Umoja wa Afrika nchini Somalia, (AUSSOM).
Afisa huyo alizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina kwa vile hajaruhusiwa kuzungumza na vyombo vya habari.
Lakini viongozi wa Somalia, aliongeza kusema kwa sasa wako tayari kufikiria upya ushiriki wa Ethiopia katika AUSSOM kufuatia mazungumzo ya maridhiano kati ya nchi zilizoandaliwa na Uturuki wiki iliyopita.
Katika miezi ya karibuni, Mogadishu ilitaka mara kwa mara Addis Ababa iondoe wanajeshi wake Somalia.
Forum