Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 16:51

Rais wa Somalia atangaza hali ya dharura nchini mwake


Mwanajeshi wa Umoja wa Afrika katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu ambao sasa unadhibitiwa na serikali na kulindwa na majeshi ya AU. August 12, 2011
Mwanajeshi wa Umoja wa Afrika katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu ambao sasa unadhibitiwa na serikali na kulindwa na majeshi ya AU. August 12, 2011

Serikali ya Somalia imetangaza hali ya dharura katika maeneo ya mji mkuu, ambayo awali yalikuwa yakidhibitiwa na kundi la wanamgambo wa ki-Islam, la al-Shabab.

Hatua hiyo ya Rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, iliyotolewa Jumamosi inasema wanamgambo wa koo wamepigwa marufuku kutoka kile alichokiita maeneo yaliyokombolewa ya Mogadishu. Serikali inajaribu kutumia mamlaka yake katika wilaya za zamani za al-Shabab ili kuzuia wababe wa kivita katika eneo hilo kuchukua udhibiti.

Serikali kwa kiasi kikubwa inawategemea wanajeshi 9,000 wa Umoja wa Afrika kuendelea kuulinda mji mkuu tangu wapiganaji wa al-Shabab walipokimbia mjini humo kiasi cha wiki moja iliyopita wakati wa mapigano na majeshi ya serikali na Umoja wa Afrika.

XS
SM
MD
LG