Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 21:52

SLAC ya Guinea yapata ushindi dhidi ya CFV Beira ya Msumbiji


Christopher Obekpa wa SLAC na Chris Crawford wakijaribu kumzuia mshambuliaji wa REG ya Rwanda.(Picha na BAL).
Christopher Obekpa wa SLAC na Chris Crawford wakijaribu kumzuia mshambuliaji wa REG ya Rwanda.(Picha na BAL).

Washindi wa mechi ya ufunguzi ya BAL ya msimu wa pili timu ya  Seydou Legacy Athletique Club (SLAC) ya Guinea wamepata ushindi mwingine dhidi ya  Ferroviario da Beira ya Msumbiji, kwa jumla ya pointi 90-74 siku ya Jumamosi.

William Perry wa Beira alitoa pasi kwa Onwuasor ambaye alipachika pointi tatu mapema katika kota ya kwanza.

Lakini Guinea ilijibu kwa pointi tatu zao wakati Crawford alipompatia pasi Obekpa ambaye aliweka mpira nyavuni.

Crawford alimpatia tena mpira Obekpa ambaye alitoa asisti kwa Nzeakor na alipachika mpira nyavuni.

Guinea iliendelea kuongoza katika kota ya pili huku Nzeakor akitoa pasi safi kwa Crawford ambaye alipachika pointi tatu ya mbali.

Mbaye wa SLAC alimpasia mpira Crawford ambaye alitengeneza pointi nyingine tatu akisukuma uongozi wao hadi pointi 10.

Kennedy wa Beira alijaribu kwa umbali mrefu wa pointi tatu na kukosa lakini Chinvelu alichukua fursa hiyo kupachika pointi mbili.

Ikiwa imesalia dakika moja tu kota ya tatu kumalizika na wakiwa chini kwa pointi 16, Kennedy alimpasia Nurmamade aliyeweka nyavuni pointi tatu.

Perry alimpatia pasi Kennedy ambaye alimpatia Nurmamade ambaye alipachika pointi tatu nyingine.

Lakini mfungaji hatari Crawford wa Guinea alipachika pointi tatu katika kota ya nne na kuendeleza uongozi hadi pointi 12.

Clube Ferroviario da Beira ya Msumbiji haikuweza kufua dafu mbele ya Seydou Legacy Athletique Club (SLAC) ya Guinea ambayo ilimaliza mchezo huo kwa ushindi wao wa pili msimu huu.

XS
SM
MD
LG