Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 04, 2025 Local time: 13:52

Siku ya ulemavu wa ngozi yaadhimishwa Kenya, Tanzania


Maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu wa ngozi yafanyika Afrika Mashariki
Maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu wa ngozi yafanyika Afrika Mashariki

Maadhimisho ya watu wenye ulemavu wa ngozi yalifanyika Mombasa na miji mingine nchini Kenya siku ya Jumanne.

Kulikuwa na tamasha za hapa na pale kwenye sherehe mbali mbali mjini Mombasa.

Nchini Tanzania, maadhimisho kama hayo yalifanyika mkoani Mbeya, lakini bila ya kuwepo walengwa.

Gazeti la Mwananchi kwa madai ya ukosefu wa fedha kwa ajili ya nauli ya kuwasafirisha, kutoka maeneo wanayoishi.

Akizungumza katika maadhimisho yaliyofanyika katika hospitali ya rufaa Kanda ya Mbeya, Kaimu Ofisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Mbeya, Grace Ngairo alisema hali hiyo imetokana na ukosefu wa bajeti.

Aidha alisema kuwa taarifa ya kufanyika maadhimisho hayo ilichelewa kuwafikia walengwa.

"Barua ya taarifa kwa ajili ya maadhimisho hayo imekuja kwa kuchelewa, lakini pia kwa sasa hakuna bajeti ya maadhimisho kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, hivyo tumeshindwa kuwasafirisha walengwa kwa ajili ya kushiriki siku yao," alisema.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika mjini Mombasa, Salma Mohamed, alifuatilia matukio kwenye sherehe hizo na kutayarisha taarifa ifuatayo;

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:48 0:00


XS
SM
MD
LG