Siku ya Haki ya Kujua ilitangazwa kwa mara ya kwanza mjini Sofia Bulgaria hapo Septemba 28 2002, wakati wa mkutano wa wanaharakati wanaotetea haki za kupata habari kutoka kwa serikali.
Tangu siku hiyo mashirika yasio ya kiserikali, wanaharakati, wasomi waandishi habari na maafisa wa serikali kote duniani hushrehekea siku hii kwa kuanda, mikutano, warsha, na kuchapisha ripoti zinaozhusiana na haki za kupata habari.
Mjini Dar es Salaam mkutano wa siku mmoja ulifanyika kujadili namna ya kuwahamasisha maafisa wa serikali kutoa habari zinazohusiana na maendeleo na usalama kwa umaa.
Deus Kibamba mkuu wa Kituo cha Taarifa kwa Wananchi nchini Tanzania, TCID, anasema moja kati ya matatizo makubwa huko Tanzania ni ukosefu wa sheria kutekeleza haki hiyo ya kikatiba.