Waziri wa elimu, Farah Sheikh Abdulkadir, amesema wizara yake inapanga kurejesha masomo katika maeneo ambayo yametwaliwa na serekali toka mwezi Agosti.
Amesema serekali imeshapeleka vifaa vya shule katika jimbo la Hirshabelle ambalo lilikuwa kiini cha mapambano dhidi ya wanamgambo.
Abdulkadir amesema ni asilimia 24 ya Wasomalia ambao kwa sasa wana fursa ya kupata elimu.
Ahadi hiyo ya kurejesha masomo katika maeneo yaliyokuwa chini ya Al Shabab ni ya kimkakati.
Imetolewa ikiwa takriban wiki tatu baada ya mabomu mfululizo kufyatuliwa yakilenga wizara ya elimu mjini Mogadishu na kuua watu 121 na kujeruhi wengine 330.