Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 08, 2024 Local time: 03:07

Shughuli za kuwatafuta manusura zinaendelea Uturuki na Syria baada ya tetemeko kubwa kuua zaidi ya watu 7,200


Wafanyakazi wa idara za dharura wakimuokoa mwanamke nje ya mabaki ya jengo lililoanguka huko Elbistan, kusini mwa Uturuki. Feb 7, 2023.
Wafanyakazi wa idara za dharura wakimuokoa mwanamke nje ya mabaki ya jengo lililoanguka huko Elbistan, kusini mwa Uturuki. Feb 7, 2023.

Timu za waokoaji nchini Uturuki na Syria Jumanne ziliendelea kuwatafuta manusura waliofukiwa kwenye vifusi vya majengo yaliyoangushwa na matetemeko makubwa ya ardhi yaliyokumba eneo hilo Jumatatu, na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 7,200.

Baada ya usiku ambapo vipimo vya hali ya hewa vilipungua hadi kwenye hali ya baridi, kulikuwa na mitetemeko mingi zaidi siku moja baada ya tetemeko hilo la kipimo cha 7.8.

Zaidi ya mitetemeko 20 kati ya hiyo ilikuwa na kipimo cha 4.0 au zaidi, na kutikisa eneo lililo kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus ameelezea uungaji wake mkono kwa wanainchi wa Uturuki na Syria katika “kipindi hiki cha huzuni mkubwa,” na amesema idadi ya vifo haizingatii “huzuni na hasara zinazopitia familia hivi sasa ambazo zimepoteza baba, mama, binti, mtoto chini ya vifusi, au ambazo hazijuwi kama wapendwa wao wako hai au wamekufa.”

Akizungumza kwenye mkutano wa WHO mjini Geneva, Tedros amesema shirika hilo linatuma ndege za kukodi na vifaa vya matibabu kwa nchi zote mbili na kwamba litafanya kazi kuwasaidia watakapopata afueni na kujenga upya.

XS
SM
MD
LG