Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 12:43

Kenya yapitisha marekebisho ya sheria tata ya uchaguzi


Sehemu ya ukumbi wa kuthibitisha matokeo ya uchaguzi Bomas Kenya. 2013.
Sehemu ya ukumbi wa kuthibitisha matokeo ya uchaguzi Bomas Kenya. 2013.

Muungano wa Jubilee ulipata kura 24 na kuwashinda mahasimu wao muungano wa CORD waliopata kura 19 katika awamu ya tatu ya upigaji kura ambapo mswaada huo uliamuliwa.

Majuma mawili baada ya bunge la taifa nchini Kenya kupitisha marekebisho ya sheria tata ya uchaguzi, hatimaye baraza la seneti lililo na idadi kubwa ya wawakilishi kutoka upande wa serikali limepitisha mswaada huo kwa kura nyingi bila ya mabadiliko yeyote.

Mwandishi wa VOA, Kennedy Wandera amesema hatimaye hili liliafikiwa baada ya maseneta hao kutofautiana vikali kuhusu ripoti ya bunge iliyokusanya maoni ya wakenya .

Kama Rais Uhuru Kenyatta ataweka saini huo mswada kuwa sheria Mfumo huo wa kuhesabu kura kupitia mkono wakati wa uchaguzi utatumika iwapo mitambo ya kielektroniki itafeli.

Hamna ishara yoyote kuwa Bwana Kenyatta atakaidi kutia sahihi mswada huo japo amepata shinikizo kutoka kwa wakenya mbalimbali yakiwemo mashirika ya kidini yanayomtaka kutoipitisha sheria hiyo wakati upinzani ulitishia kuitisha maandamano iwapo mabunge hayo mawili yatapitisha marekebisho ya sheria hizi za uchaguzi.

Hatimaye baada ya majadiliano makali maseneta walipitisha mswaada huo ambapo wale wa upande wa serikali wa muungano wa Jubilee walipata kura 24 na kuwashinda mahasimu wao CORD waliopata kura 19 katika awamu ya tatu ya upigaji kura ambapo mswaada huo uliamuliwa.

Kutokana na wingi huo wa kura, sasa mswaada huo ambao umezua ukinzani mkubwa wa kisiasa, utakabidhiwa kwa rais Uhuru Kenyatta kwa kuweka saini ilikuwa sheria.

Bunge la taifa lilipitisha mswaada huo wiki mbili zilizopita. Katika mswaada huo, wabunge hao walieleza kuwa ni sharti pawepo mfumo usiokuwa wa kielektroniki kama njia mbadala iwapo mitambo itaatilika wakati wa uchaguzi mkuu.

Desemba 22 mwaka jana, baraza la seneti liliitisha kikao maalum cha maseneta kujadili sheria hizo za uchaguzi ambazo zilizua hisia kali za kisiasa baada ya kupitishwa kwake na bunge la taifa.

Katika kutafuta muafaka maseneta walikubaliana kuunda kamati ya pamoja kutoka pande mbili kuu za kisiasa na kuandaa kikao kukusanya maoni kutoka kwa wakenya kuelezea hisia zao kuhusu mapendekezo ya sheria hizo.

Kufuatia maoni ya wakenya kuhusu mapendekezo ya kutumia mfumo usiokuwa wa kielektroniki, mabishano makali yalizuka huku maseneta wa muungano wa Jubilee na CORD wakionekana kugawanyika katika misingi ya kisiasa kuhusu ripoti hiyo.

Seneta Mteule Janet Ong’era alitupilia mbali mapendekezo ya sheria hizo na kusema kuwa hivi vilikuwa tu vigezo vinavyoletwa na Jubilee kufanya hila katika uchaguzi mkuu.

Kiongozi wa walio wachache katika seneti, Moses Masika Wetang’ula alisisitiza kuwa mswaada huu unaenda kinyume na katiba na hivyo basi huenda ukaitwaa nchi katika ghasia zilizoshuhudiwa mwaka wa 2007 na 2008.

Lakini maseneta wa Jubilee walionekana kutotishwa na kauli za wenzao kutoka mrengo wa upinzani. Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen, Stephen Sang(Nandi), Kembi Gitura(Murang’a),Kiraitu Murungi (Meru) walisimama kidete katika mjadala mkali wa kisiasa kutoka kwa wenzao wa mrengo wa CORD na kuunga mkono mswaada huo.

XS
SM
MD
LG