Hata hivyo, Ukraine inajaribu kusafirisha nafaka yake kwenye bahari inayodhibitiwa na wanachama wa NATO, Bulgaria na Romania. Meli hiyo yenye bendera ya Palau ilikuwa inaelekea Misri.
Wateja wa mafuta ya petroli na dizeli nchini Russia kuna uwezekano mkubwa wa kukabiliwa na uhaba wa bidhaa hizo ndani ya nchi, wizara ya ulinzi ya Uingereza imesema Jumapili katika taarifa yake ya kila siku ya kijasusi kuhusu uvamizi wa Russia nchini Ukraine.
Wizara hiyo imesema Russia ilisitisha karibu mauzo yote ya dizeli na petroli siku ya Alhamisi “ ili kuweka uwiano kwenye masoko yake ya ndani.”
Hatua hiyo kulingana na wizara hiyo, itaendelea kwa “uhakika kupunguza” usambazaji wa bidhaa hizo kote ulimwenguni.
Wizara hiyo imesema, nchi ambazo zinategemea mafuta ya Russia ndizo zitaathirika zaidi na hatua hiyo.
Forum