Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 10:44

Shambulio la risasi kwenye duka kubwa laua watu 3 mjini Copenhagen


Ramani ya Denmark
Ramani ya Denmark

Shambulio la risasi katika jengo la maduka mjini Copenhagen Jumapili limesababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi wengine watatu, polisi wa Denmark wamesema, wakiongeza kuwa wamemkamata mshukiwa wa shambulio hilo raia wa Denmark mwenye umri wa miaka 22.

Picha kutoka eneo la tukio zimeonyesha wazazi wakibeba watoto wao walipokuwa wanakimbia kutoka jengo lililoshambuliwa, huku wafanyakazi wa gari la kubeba wagonjwa wakiwabeba watu kwenye machela.

“Tunajua kwamba kuna watu 3 waliouawa,” mkuu wa polisi wa Copenhagen Soren Thomassen ameuambia mkutano wa waandishi wa habari Jumapili asubuhi, akiongeza kuwa kuna pia wengine watatu waliojeruhiwa.

Thomassen amemuelezea mshukiwa aliyekamatwa kuwa ni raia wa Denmark, mwenye umri wa miaka 22, lakini bado ni mapema sana kujua sababu ya shambulio hilo.

“Tunachunguza kitendo hicho, na inawezekana kuwa ni ugaidi,” mkuu huyo wa polisi amesema.

Ameongeza kuwa hakuna ishara kwamba mtu huyo alifanya kitendo hicho kwa kushirikiana na wengine, na polisi waliimarisha ulinzi kando na duka hilo na mjini kote Copenhagen.

Shambulio hili linatokea wiki moja baada ya shambulio jingine kama hilo katika nchi Jirani ya Norway ambako watu wawili waliuawa na mshambuliaji moja mjini Oslo.

XS
SM
MD
LG