Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 16:13

Shambulio la Israel dhidi ya Iran liliharibu vituo viwili vya kijeshi vya Iran


Jeshi la Israel limeshambulia vituo vya kijeshi vya Iran.
Jeshi la Israel limeshambulia vituo vya kijeshi vya Iran.

Baadhi ya majengo yaliyoharibiwa yako  katika kambi ya kijeshi ya Parchin nchini Iran, ambako shirika la IAEA liliishuku  Iran

Shambulio la Israel dhidi ya Iran liliharibu vituo viwili vya kijeshi kusini mashariki mwa mji mkuu wa Iran, kulingana na picha za satelaiti zilizo-onyeshwa Jumapili na shirika la habari la Associated Press.

Katika siku za nyuma, wataalamu walilihusisha eneo moja na mpango wa silaha za nyuklia wa Tehran na jingine na mpango wake wa makombora ya masafa marefu.

Baadhi ya majengo yaliyoharibiwa yako katika kambi ya kijeshi ya Parchin nchini Iran, ambako Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki-IAEA liliishuku Iran, katika siku za nyuma ilifanya majaribio ya milipuko mikubwa ambayo inaweza kusababisha utengenezaji silaha za nyuklia.

Iran kwa muda mrefu imekuwa ikisisitiza kuwa mpango wake wa nyuklia ni kwa malengo ya amani, ingawa shirika la IAEA, mashirika ya upelelezi ya Magharibi na mengine yanasema Tehran ilikuwa na program ya silaha iliyo hai hadi mwaka 2003.

Uharibifu mwingine unaweza kuonekana katika kambi ya karibu ya kijeshi ya Khojir, ambayo wachambuzi wanaamini inaficha mfumo wa handaki la chini ya ardhi pamoja na maeneo ya uzalishaji wa makombora.

Forum

XS
SM
MD
LG