Vyombo vya habari vya serikali vimeripoti kwamba maafisa wa usalama waliwadhibiti kwa mafanikio wanamgambo ambao walisambulia hoteli ya Pearl Beach Ijumaa jioni na kuokoa idadi kubwa ya raia.
Polisi wa Somalia wamesema watu tisa waliuawa na wengine 10 kujeruhiwa katika shambulio hilo.
Katika taarifa, idara ya polisi imesema waliouawa ni raia sita na maafisa watatu wa usalama.
Polisi wamesema pia kwamba watu 84 wakiwemo watoto, wanawake na wazee, waliokolewa kutoka eneo la shambulio.
Mashahidi wameiambia idhaa ya Kisomalia ya Sauti ya Amerika kwamba shambulio lilianza kwa milipuko miwili nje ya hoteli ya Pearl Beach, lilifuatiwa na watu wenye silaha walioivamia hoteli hiyo.
Milio ya risasi ilisikika huku kukiwa idadi isiyojulikana ya watu waliokwama ndani ya jengo hilo, mashahidi wamesema, huku wengine wakifanikiwa kutoroka kupitia milango ya nyuma na madirisha.
Kundi la Al-Shabaab, lenye uhusiano la Al-Qaida limekiri kufanya shambulio hilo.
Forum