Serikali ya Sudan imesema kuwa itatuma ujumbe wake Cairo kwa majadiliano na maafisa wa Marekani na Misri siku ya Jumatatu wakiendelea kuweka wazi swali kuhusu kushiriki katika mazungumzo ya amani yanayolenga kumaliza vita vya miezi 16.
Serikali inayodhibitiwa na jeshi ambalo linapigana na wanamgambo wa kikosi Rapid Support Forces (RSF) kwa ajili ya udhibiti wa nchi inasema haitoshiriki katika mazungumzo ya Amani huko Uswizi, hadi makubaliano ya awali yaliyokwama huko Jeddah yanatekelezwa.
Mazungumzo yanayoongozwa na Marekani, ambayo RSF inahudhuria yanalenga kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoibuka Aprili 2023 na kupelekea mzozo wa kibinadamu ambao umesababisha nusu ya watu nchini Sudan milioni 50 kukabiliwa na ukosefu wa chakula.
Forum