Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 17:10

Serikali ya Sudan imeachilia huru wapinzani wawili wa mapinduzi ya kijeshi siku moja baada ya kukamatwa


Waandamanai wa Sudan wakipinga ukandamizaji.
Waandamanai wa Sudan wakipinga ukandamizaji.

Chama cha Communist cha Sudan kimesema kwamba serikali mapema Ijumaa imeachilia huru wapinzani wawili wa mapinduzi ya kijeshi siku moja baada ya kukamatwa.

Chama cha Communist cha Sudan kimesema kwamba serikali mapema Ijumaa imeachilia huru wapinzani wawili wa mapinduzi ya kijeshi siku moja baada ya kukamatwa.

Mapinduzi ya kijeshi ya Oktoba mwaka jana nchini humo yamezua maandamano ya kitaifa na kupelekea msako mkali uliosababisha vifo vya takriban watu 95 huku mamia wengine wakijeruhiwa kulingana na ripoti kutoka muungano wa madaktari.

Mamia ya watu pia wamezuiliwa tangu maandamano ya kuitisha utawala wa kiraia yalipoanza. Maafisa wa usalama jana Alhamisi waikamata na kumzuilia katibu wa kisiasa wa chama cha Communist Mohammed Mukhtar ala Khatib akiwa na mwanachama mwingine wa ngazi ya juu.

Wawili hao walikamatwa baada ya kukutana na kiongozi wa uasi Abdel Wahid Nour ambaye awali alikataa kutia saini mkataba wa kihistoria wa amani wamwaka wa 2020 kati yao na serikali ya Sudan.

Umoja wa Mataifa pamoja na Umoja wa Afrika zimeendelea kuomba mazungumzo kufanyika kati ya pande zote zinazozozana nchini humo. Mapinduzi ya mwaka jana nchini humo yamechochea ukososji mkubwa wa kimataifa tangu yalipofanyika.

XS
SM
MD
LG