Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:16

Nigeria yathibitisha kupotea wasichana 110


Wasichana wa shule 110 wamepotea Nigeria
Wasichana wa shule 110 wamepotea Nigeria

Serikali ya Nigeria imethibitisha Jumapili kwamba wasichana 110 wamepotea baada ya wanamgambo wa Boko Haram kushambulia mji mmoja uliopo kaskazini-mashariki.

Wizara ya habari ilisema wasichana kutoka chuo cha serikali cha sayansi na ufundi huko Dapchi katika jimbo la Yobe hawaonekani baada ya washukiwa wanamgambo wa Boko Haram kuvamia shule yao siku ya Jumatatu. Lakini siku kadhaa zilikuwa zimepita kabla ya maafisa wa serikali kutoa tamko hilo.

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari
Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari alisema Jumapili kwamba ndege za jeshi za ziada pamoja na vikosi vilivyokuwepo katika eneo la tukio vimeanza kuwatafuta wasichana hao waliopotea. Wapiganaji wenye silaha nzito wakiwa kwenye magari walishambulia mji wa Dapchi siku ya Jumatatu jioni inaripotiwa kwamba katika uvamiaji huo walikuwa wakiwataka wasichana wa shule pekee.

Awali maafisa walikanusha shutuma za wasichana hao kutekwa nyara wakisisitiza kwamba walikuwa wamejificha vichakani baada ya shambulizi.

XS
SM
MD
LG