Serikali imekuwa katika mzozo mkubwa na waasi, lakini katika wiki za hivi karibuni pande zote mbili zimesisitiza uwezekano wa mazungumzo ya kumaliza vita vya miezi 21, huku Ethiopia ikishinikiza Umoja wa Afrika kuongoza mazungumzo yoyote.
Waasi kwa upande wao wanamtaka Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, ambaye amekuwa akihusika sana katika juhudi za amani, kuwa mpatanishi kati ya pande hizo mbili.
Mjumbe wa Umoja wa Afrika katika pembe ya Afrika Olusegun Obasanjo ambaye amekuwa akiongoza harakati za kidiplomasia za kumaliza mzozo huo, ametoa taarifa kwa Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika kuhusu hatua hiyo iliyofikiwa.
Katika taarifa ya tarehe 4 Agosti lakini ambayo ilichapishwa kwenye tovuti ya Umoja wa Afrika Jana Alhamisi, Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika limesema “ linapongeza uwakilishi wake mkuu kwa majadiliano ya moja kwa moja kati ya serikali kuu ya Ethiopia na chama cha Tigray’s People Liberation Front( TPLF).
Ni taarifa ya kwanza iliyowekwa hadharani ya mawasiliano ya moja kwa moja kati ya serikali ya waziri mkuu Abiy Ahmed na TPLF, ambayo kiongozi wake Debretsion Gebremichael alisisitiza kwamba huduma muhimu zapaswa kurejeshwa huko Trigray kabla ya mazungumzo kuanza.