Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:56

Serikali ya Burundi Yasusia Mazungumzo ya Arusha


Rais Pierre Nkurunziza
Rais Pierre Nkurunziza

Serikali ya Burundi imetoa tamko Jumatano kwamba haitapeleka ujumbe wake katika mazungumzo ya Burundi huko Arusha, Tanzania.

Mazungumzo juu ya kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa wa Burundi yanatarajiwa kuanza Alhamisi, lakini kuna wasiwasi ulioenea kwamba mazungumzo hayo hayatasaidia kuleta amani katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati inayokabiliwa na mgogoro wa kisiasa.

Wapinzani na asasi za kiraia wanasema msimamizi wa mazungumzo hayo, rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa, anavuruga mchakato huo kwa kuwakaribisha wanasiasa ambao walifanya jaribio la kumpindua Rais Pierre Nkurunziza mwaka 2015.

XS
SM
MD
LG