Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 30, 2024 Local time: 12:15

Serekali ya kijeshi la Mali yatangaza kuruhusu shughuli za kisiasa


Serikali ya kijeshi ya Mali imetangaza Jumatano imekuwa ikitoa tena idhini kwa vyama na shughuli za kisiasa ambazo zilisitishwa mwezi Aprili.

“Serikali imeamua kuondoa marufuku ya vyama vya siasa na shughuli zake,” imesema taarifa ya baraza la mawaziri ambalo linatawaliwa na viongozi wa kijeshi waliochukua madaraka katika mapinduzi ya 2020.

Mkuu wa serikali ya kijeshi, Kanali Assimi Goita, alihalalisha kusimamishwa kile alichokiita upotoshaji wa vyama vya siasa, ambao ulikuwa hatari kwa mazungumzo yanayoendelea ya kitaifa kuhusu mustakabali wa kisiasa wa Mali.

Vyama hivyo wakati huo vilikuwa vinapinga uamuzi wa kanali wa kubaki madarakani kwa zaidi ya Machi 2024 na kutaka kurejea utawala wa kiraia.

Vyama vya upinzani vilisusia mazungumzo ambayo yaliendelea na wafuasi wa serikali, ambao Mei walitoa mapendekezo ya wanajeshi kubaki madarakani kwa miaka miwili hadi mitano ya ziada, na kiongozi wa sasa aruhusiwe kushiriki uchaguzi wowote ujao wa urais.

Forum

XS
SM
MD
LG