Na Kennes Bwire
Kampala, Uganda
Mahakama kuu ya Uganda, imeamrisha mahakama ya kijeshi kusimamisha shughuli ya kusikiliza kesi ya aliyekuwa kiongozi wa ujasusi nchini humo, Generali David sejjusa, kwa msingi kwamba mahakama hiyo ya kijeshi haina mamlaka ya kumhukumu.
Jaji Margret Ogoli, akitoa kauli hiyo mjini Kampala, amesema kwamba mahakama ya kijeshi inavunja sheria kwa kuendelea kusikiliza kesi yake Sejjusa, pamoja na kumnyima dhamana.