Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 05:54

Scholz yupo Kenya kwa ajili ya miradi ya nshati na mazingira


Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz PICHA: Reuters
Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz PICHA: Reuters

Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz amewasili Nairobi Kenya kwa ziara ya kikazi inayoangazia nshati safi na utunzaji wa mazingira.

Scholz amesema kwamba anatambua kwamba kuna uwezekano wa kupata ushirikiano na serikali ya Kenya kuhusu matumizi ya nshati safi na namna ya kulinda mazingira.

Kenya ni mshirika mkubwa kibiashara na Ujerumani na inapanga kuhakikisha kwamba inatumia nshati safi isiyo na madhara kwa mazingira ifikapo mwaka 2030.

Viongozi wa ujerumani wamekuwa wakiingia makubaliano na nchi kadhaa, yanayohusiana na nshati baada ya kulazimika kuanza uagizaji wa ncshati kutoka Russia baada ya kuanza kwa vita vya Ukraine.

Hii ni mara ya pili Scholz anatembelea Afrika tangu alipoingia ofisini Desemba 202.

Ziara yake ni ishara ya umuhimu ambao mataifa ya magharibi yametoa kwa Afrika wakati yanalenga kumaliza ushawishi wa China na Russia barani humo.

XS
SM
MD
LG